dailyhabari

Daily News/HabariLeo blog

MAMA SALMA KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUNAWA MIKONO DUNIANI


Baadhi ya watoto pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za mkoa wa Dar es salaam wakipita mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani  leo. Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) ndiye aliyekuwa mgeni kwenye sherehe hizo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar leo
  
 Watoto wakicheza ngoma ya msewe ya Zanzibar
 Wasanii wa Kikundi cha Orijino Comedy kikionyesha zoezi la kunawa mikono wakati wa maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani lililofanyika leo  jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete hayupo pichani
 Mama Salma Kikwete akiwaonyesha watoto zoezi la jinsi ya kunawa mikono kwa sabuni wakati wa maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani 
 Sehemu ya tukio lilifanyika sherehe ya maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani 
 Baadhi ya watoto wa shule za msingi jijini Dar es Salaam wakiangalia aina ya kibuyu chirizi ambacho hutumika kuweka maji kwaajili ya kuoshea mikono.
Watoto wakitoa burudani.
Picha na Mwanakombo Jumaa – MAELEZO

October 16, 2011 Posted by | Habari | Leave a comment

Timu za Burundi zang’ara katika mashindano ya kanda ya 5 ya mpira wa kikapu


 Mchezaji wa timu ya Co-operative ya Kenya, Mark Mayen akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa Urunani ya Burundi, Niagunduka Donde katika mchezo wa fainali ya mashindano ya kanda ya tano ya mpira wa kikapu iliyomalizika usiku huu kwenye uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es Salaam
 Washindi wa Pili timu ya Co-Coperative Bank ya Kenya
 Mashabiki wa timu ya Burundi
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Leonard Thadeo (shoto) akimkabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya kanda ya tano ya mchezo nahodha wa timu ya Urunani ya Burundi leo
 mashabiki wa timu ya Urunani ya Burundi wakisherehekea ubingwa
 Mabingwa wa kanda ya tano wa mpira wa kikapu timu ya Urunani ya Burundi.
Wachezaji wa timu ya Burundi wanawake na wanaume wakiwa katika picha ya pamoja. 

October 16, 2011 Posted by | michezo | Leave a comment