Habari katika Picha

Mke wa Rais, Salma Kikwete akisalimiana na mke wa rais wa Uganda, Jane Mseveni

Spika wa Bunge la Jamuhuli ya Muungano, Samuel Sitta(kushoto) akisalimiana na Viongozi wa (UWT) wa Manispaa ya Kinondoni, walipotembelea Bunge baada ya kualikwa na Mh, Idd Azan (wenye tai)

Meli ya mizingo ya Mv. Pemba ikiwaka moto katika bandari ya Dar es Salaam jana.

Mke wa Rais, Salma Kikwete akizungumza na mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland, Malkia Matsebula Mjini Kampala, Uganda.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kaigara,wilaya ya Muleba muda mfupi baada ya Mama Salma.

Rais Jakaya Kikwete(kulia) na Mfalme Mswati III wa Swaziland wakiingia katika ukumbi wa mkutano wa Hoteli ya Speke's Bay Resort iliyoko Munyonyo jijini Kampala, Ugnada.

Mwanafunzi Milembe Zakaria anayesoma katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Rugambwa iliyopo mjini Bukoba,mkoani Kagera akimvika skafu Mama Salma Kikwete muda mfupi baada ya Mama Kikwete kuwasili shuleni hapo ambapo aliongea na wanafunzi hao.

Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiagana na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rugambwa mjini Bukoba,mkoani Kagera muda mfupi baada ya kuongea na wanafunzi hao shuleni hapo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amembeba Mtoto Elisha ambaye ni mtoto wa Bi.Mariam Stanford mlemavu wa ngozi(albino) kutoka Ngara wakati Mama Kikwete alipokutana na wawakilishi wa SACCOS za Mkoa wa Kagera

Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya jumla ya shilingi Milioni Tano 5m/- kwa viongozi wa Vyama Vya akiba na kukopeshana SACCOS vya mkoa wa Kagera.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete awaenzi Mashujaa wa Vita vya Kagera
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana na Mzee David Musuguri katika makaburi ya Mashujaa wa vita vya Kagera huko Kaboya, wilayani Muleba Mkoani Kagera Jumamosi. Chini wakiweka shada la maua katika mnara wa Mashujaa hao 

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika huko Kaboya mkoani Kagera Jumamosi hii.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakikagua baadhi ya Makaburi ya Mashujaa wa vita vya Kagera huko Kaboya, wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Mwenyekiti kamati ya Bunge Maendeleo ya Jamii, Jennista Mhagama akijadili jambo na Mkurungezi Mkuu wa NSSF Ramadhani Dau.

Mchuuzi akisukuma mkokoteni wenye mizigo kutoka Ilala kwenda Kariakooo katika barabara ya Uhuru.

Watoto wakiwa wamepanda juu ya mkokoteni wenye Ng'ombe.
-
Recent
-
Links
-
Archives
- July 2009 (27)
- June 2009 (117)
- May 2009 (40)
- April 2009 (36)
- March 2009 (17)
-
Categories
-
RSS
Entries RSS
Comments RSS


